Mkenya Mdadisi

Blogu kuhusu siasa za Kenya, uchumi, dini, fasihi, vyombo vya habari, tamaduni, jamii na kiwacho chote kitakachonipendeza. Wakati mwingine sibashiriki, walakin natumai utachangamka kadri ninavyolekea ninakoamini ni sawa. - Jesse Masai, Mmiliki & Mhariri Mkuu. --------------------------------------- WAWEZA KUNIFIKIA KWA KUTUMIA ANWANI HII: Kenyananalyst@yahoo.co.uk (c) Jesse Masai, 2006

Tuesday, May 16, 2006

"Tumekushiba," Wabunge wamwambia Obasanjo


Wanaijeria wamlipa sawa na tamaa yake....

Sunday, May 14, 2006

Ni nani atakayemsaidia "Bi. Savimbi?"


Kwa kawaida siblogu kuhusu siasa za Kenya au kimataifa, ila yaelekea kuna mtu ambaye kidogo angali anatambua kuwa ninapendelea maswala ya siasa na historia...na kwamba ningali nina kumbukumbu ya Waafrika wanaokumbukwa katika historia. Marehemu Jonas Savimbi ana nafasi yake kati ya watu ninaowakumbuka, kutokana na kwamba nilifuatia kwa karibu maisha yake ya kibinafsi, kisiasa na kijeshi. Hivi hapana kioja au kiroja kinachoweza kushinda barua hii ya uongo niliyoipokea asubuhi ya leo kutoka kwa mtu - ninayemdhania kuwa Mnaijeria - anayedai kuwa mkewe. Mwenzako naomba umsaidie :-)
Subject:  Mrs. Nancy Savimbi (Angola Unita)

My Dear Friend

I am Mrs.Savimbi, the wife to the late Jonas Savimbi, the late leader
of the national Union for The Total Independence of Angola (UNITA). My
husband was killed during combat action against government forces in
Mexico, Angola on the 22nd of Feb. 2002.

I am contacting you because of my need to deal with person whom my
family had no previous relationship.Since the death of my husband, my
family has been subjected to all sorts of harassment and intimidation with
lots of negative report emanating from the government of President
Santos about my husband.

The present government has also ensured that all our bank accounts are
frozen, and all assets sized.It is in view of this that I seek your
assistance in investing and managing the sum of Seventy five Million
United State Dollars in your country, being the very last of my family funds
in my possession and control unknown to the government.This money now
in question came as a result of Diamond Royalties that was paid to my
late husband from the Diamond mining within the areas in Angola being
controlled by (UNITA) for more than a decade.

The money was packed in a sealed trunk box and was depositd
Security/Finance Company in Spain.Right now, the present government has
intensified their probe on my family's financial resources; frozen all our known
foreign & local accounts, revoked Diamond licenses, and even detained
my son (Charles) on alleged flimsy charges just because my husband
before his death was the head of UNITA.Bearing in mind that your assistance
is needed to transfer this money, I propose a commission of 10% (Ten
Percent) of the total sum to you or your company for the expected
services and assistance.

Please reply me through this email address below for security reasons:
nancysavimbi@myway.com


I await your prompt response to commence the transaction process.


Mrs.Nancy Savimbi
nancysavimbi@myway.com
Picha ni kwa hisani ya BBC Online

Saturday, May 13, 2006

Maelezo zaidi kufuatia shambulio dhidi ya kitua cha redio jijini Nairobi

Bonyeza hapa.

Friday, May 12, 2006

Homa ya kuku na kufilisika kwa bunge la Afrika


Muda mfupi uliyopita ndugu Msangi amenijuza habari za homa ya kuku kufika Djibouti na bunge la Umoja wa Afrika kufilisika.
Kwa vile sikuwa nimetilia maanani habari nyingi leo, niligutuka kidogo...na hapa basi ndiyo mawazo yangu ya muda kuyahusu mambo hayo.
- Homa ya kuku: Ni dhana yangu kuwa huenda nchi nyingi za Afrika zina tatizo hilo, ila huenda zimenyamaza kwa hofu ya kuwapoteza watalii ambao ni vitega uchumi muhimu. Mwenendo wa nchi nyingi barani umekuwa ni kumficha mgonjwa kisha baadaye kushindwa kuficha vilio anapoiaga dunia. Ni uzalendo wa kipumbavu, iwapo utauliza maoni yangu.
- Bunge la Afrika - Itakuwa aibu iliyoje iwapo wataenda kuombaomba ugenini katika enzi hizi za "kujitawala" na "kujitegemea!" Kuna wakati mwenzetu Gadaffi alijitolea kulipa madeni ya baadhi ya nchi za Afrika kwa uliyokuwa Umoja wa nchi huru za Kiafrika (OAU)...wakati alipokuwa akikampeini kuwa mwenyekiti wa umoja huo....pengine Umoja uliopo sasa wahitaji tena huo ukarimu wake. Ila pia Gadaffi kwangu ni sarafu isiyoaminika...mara yuko huku kwetu, mara yuko kwenye baraza la nchi huru za Kiarabu, mara...hata simwelewi siku zingine. Anawafahamu Waarabu, amekuwa nao tangu 1969 hivi (alipoingia madarakani). Nafikiri pengine ni mkengeuko wa kisiasa katika Afrika ambao ndiyo kidogo unamtatiza.
Asante ndugu Msangi kwa kunichochea kiasi hiki :-)
*Namshukuru mamangu kwa picha hiyo...nje ya pale ninapopaita nyumbani.

Thursday, May 11, 2006

Wokovu sasa "umerahisishwa"

Bonyeza hapa kwa habari zaidi.
Pia nimeweka kiunganishi hicho kwenye blogu yangu ya Kiingereza (chini ya vyombo vya habari nchini Kenya na ulimwenguni)...ukipate cha kufaa kwako au kwa awaye yote siku zijazo.
Nitakiweka kwenye blogu hii kabla ya siku hii kuisha kwa majaliwa.

Sehemu ya tano ya majibu kwa "Kifo cha Ibilisi"

Bonyeza hapa kwa habari hizo.

Maelezo zaidi:

Habari za utangulizi wa mjadala huu
Mjadala (katika lugha ya Kiswahili)
Sehemu ya kwanza ya majibu
Sehemu ya pili ya majibu
Sehemu ya tatu ya majibu
Sehemu ya nne ya majibu

Wednesday, May 10, 2006

Kanisa jijini Zurich, Uswizi

Grace, mkenya anayeishi Uswizi, ameniandikia kusema kuwa Path of Life ni kanisa ambalo huenda likamfaa awaye yote atakayekuwa akizuru nchi hiyo.
Tukio hilo limenifanya kuanzisha sehemu tatu maalum za habari kuhusu pale mtu anaweza kuhudhuria ibada za Jumapili nchini Kenya, bara Ulaya na Marekani.
Nitazirefusha orodha za makanisa hayo kadri nitakavyopata mapendekezo zaidi toka kwenu; nitazingatia kadri kanisa unalopendekeza linavyojimudu kuishia malengo na maono yake ya imani.
Kanisa lolote linaloambatana na maelezo ya imani yangu litapata nafasi mara moja.

Muziki na gumzo za Kikalenjin kwenye tovuti

Na KIP

Hii ni kuwajulisheni kuwa kuna muziki mpya kwenye tovuti yangu.
Naomba unisaidie kusambaza ujumbe huo.
Pia tembelea tovuti yenye mijadala katika lugha ya Kikalenjin.
Asante.

Tuesday, May 09, 2006

Sehemu ya nne ya majibu kwa "Kifo cha Ibilisi"

Bonyeza hapa ili upate habari za sehemu hiyo.

Maelezo zaidi:

Habari za utangulizi kwa mjadala huu
Mjadala
Sehemu ya kwanza ya majibu
Sehemu ya pili ya majibu
Sehemu ya tatu ya majibu

Nimekamilisha shughuli zangu kama mhariri wa muda. Asanteni kwa kusoma.
- Z.M, Mhariri wa muda.